Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 7 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ أُمِّ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَرۡضِعِيهِۖ فَإِذَا خِفۡتِ عَلَيۡهِ فَأَلۡقِيهِ فِي ٱلۡيَمِّ وَلَا تَخَافِي وَلَا تَحۡزَنِيٓۖ إِنَّا رَآدُّوهُ إِلَيۡكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ﴾
[القَصَص: 7]
﴿وأوحينا إلى أم موسى أن أرضعيه فإذا خفت عليه فألقيه في اليم﴾ [القَصَص: 7]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tukampa mawazo mamake Mūsā alipomzaa na akamuogopea asije Fir'awn akamchinja kama anavyowachinja watoto wa wana wa Isrāīl kwamba «mnyonyeshe ukiwa mtulivu, na pindi uogopapo kujulikana mambo yake, muweke sandukuni na ulitupe kwenye mto wa Nail bila ya kuogopa kwamba fir'awn na watu wake watamuua na bila ya kuwa na masikitiko ya kuepukana na yeye, hakika sisi tutamrudisha kwako na tutamtumiliza kuwa Mtume.» |