Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 73 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿وَمِن رَّحۡمَتِهِۦ جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ لِتَسۡكُنُواْ فِيهِ وَلِتَبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِهِۦ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ ﴾
[القَصَص: 73]
﴿ومن رحمته جعل لكم الليل والنهار لتسكنوا فيه ولتبتغوا من فضله ولعلكم﴾ [القَصَص: 73]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa rehema Yake kwenu, enyi watu, ni kuwafanyia usiku na mchana Akatafautisha baina ya viwili hivi, Akaufanya huu usiku kuwa ni giza, ili mutulie humo na miili yenu ipumzike. Na Akawafanyia mchana kuwa ni mwangaza, ili mutafute maisha yenu na ili mumshukuru Yeye kwa kuwapa nyinyi neema zake hizo |