Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 79 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوۡمِهِۦ فِي زِينَتِهِۦۖ قَالَ ٱلَّذِينَ يُرِيدُونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا يَٰلَيۡتَ لَنَا مِثۡلَ مَآ أُوتِيَ قَٰرُونُ إِنَّهُۥ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٖ ﴾
[القَصَص: 79]
﴿فخرج على قومه في زينته قال الذين يريدون الحياة الدنيا ياليت لنا﴾ [القَصَص: 79]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi akatoka Qārūn akiwa kwenye pambo lake, akitaka kwa kufanya hivyo kuonyesha ukubwa wake na wingi wa mali yake. Na walipomuona wale wanaotaka pambo la uhai wa kilimwengu walisema, «Tunatamani lau sisi tungalipatiwa mfano wa kile alichopatiwa Qārūn, cha mali, pambo na heshima. Kwa kweli, Qārūn ni mwenye sehemu kubwa ya dunia.» |