Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 78 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿قَالَ إِنَّمَآ أُوتِيتُهُۥ عَلَىٰ عِلۡمٍ عِندِيٓۚ أَوَلَمۡ يَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ قَدۡ أَهۡلَكَ مِن قَبۡلِهِۦ مِنَ ٱلۡقُرُونِ مَنۡ هُوَ أَشَدُّ مِنۡهُ قُوَّةٗ وَأَكۡثَرُ جَمۡعٗاۚ وَلَا يُسۡـَٔلُ عَن ذُنُوبِهِمُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ ﴾
[القَصَص: 78]
﴿قال إنما أوتيته على علم عندي أو لم يعلم أن الله قد﴾ [القَصَص: 78]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Akasema Qārūn kuwaambia watu wake waliomuwaidhia, «Kwa hakika, mahazina haya ya mali nimeyapata kutokana na ujuzi na uwezo.»Kwani Qārūn hajui kwamba Mwenyezi Mungu ameshawaangamiza ummah wengi kabla yake yeye waliokuwa na nguvu zaidi za kushinda na ukusanyaji zaidi wa mali? Na hawataulizwa wahalifu kuhusu dhambi zao, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Anazijua, isipokuwa wataulizwa maulizo ya kuwalaumu na kuwasimanga. Na Atawatesa Mwenyezi Mungu kulingana na ujuzi Wake kuhusu wao |