Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 85 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿إِنَّ ٱلَّذِي فَرَضَ عَلَيۡكَ ٱلۡقُرۡءَانَ لَرَآدُّكَ إِلَىٰ مَعَادٖۚ قُل رَّبِّيٓ أَعۡلَمُ مَن جَآءَ بِٱلۡهُدَىٰ وَمَنۡ هُوَ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ ﴾
[القَصَص: 85]
﴿إن الذي فرض عليك القرآن لرادك إلى معاد قل ربي أعلم من﴾ [القَصَص: 85]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika Yule Aliyekuteremshia wewe, Qur’ani, ewe Mtume, na akakulazimisha wewe uifikishe na ushikamane nayo, ni Mwenye kukurudisha kule ulikotoka, nako ni Makkah. Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Mola wangu Anamjua zaidi yule aliyeleta uongofu na yule ambaye ameenda nje ya haki waziwazi.» |