Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 19 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ كَيۡفَ يُبۡدِئُ ٱللَّهُ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥٓۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ ﴾
[العَنكبُوت: 19]
﴿أو لم يروا كيف يبدئ الله الخلق ثم يعيده إن ذلك على﴾ [العَنكبُوت: 19]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani hawa hawajui ni vipi Mwenyezi Mungu Anaanzisha uumbaji viumbe kutoka katika hali ya kutokuwako, kisha Atawarudisha baada ya kutoweka kwao, kama alivyoanzisha mara ya kwanza uumbaji mpya na kwamba kulifanya hili si jambo lisilowezekana na Yeye? Hakika hilo kwa Mwenyezi Mungu ni lepesi kama lilivyokuwa lepesi lile la kuanzisha uumbaji wake |