Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 18 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿وَإِن تُكَذِّبُواْ فَقَدۡ كَذَّبَ أُمَمٞ مِّن قَبۡلِكُمۡۖ وَمَا عَلَى ٱلرَّسُولِ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ ﴾
[العَنكبُوت: 18]
﴿وإن تكذبوا فقد كذب أمم من قبلكم وما على الرسول إلا البلاغ﴾ [العَنكبُوت: 18]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mkimkanusha, enyi watu, Mtume wetu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, katika kile alichowalingania mkifuate cha kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake, basi kuna makundi ya watu kabla yenu waliowakanusha Mitume wao katika kile walichowaitia, na kwa hivyo zikawashukia hasira za Mwenyezi Mungu. Na Mtume Muhammad hana jukumu lingine isipokuwa ni kuwafikishia nyinyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ujumbe Wake ufikishaji wenye uwazi, na ashafanya hilo |