Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 33 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿وَلَمَّآ أَن جَآءَتۡ رُسُلُنَا لُوطٗا سِيٓءَ بِهِمۡ وَضَاقَ بِهِمۡ ذَرۡعٗاۖ وَقَالُواْ لَا تَخَفۡ وَلَا تَحۡزَنۡ إِنَّا مُنَجُّوكَ وَأَهۡلَكَ إِلَّا ٱمۡرَأَتَكَ كَانَتۡ مِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ ﴾
[العَنكبُوت: 33]
﴿ولما أن جاءت رسلنا لوطا سيء بهم وضاق بهم ذرعا وقالوا لا﴾ [العَنكبُوت: 33]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Malaika walipomjia Lūṭ, hilo lilimkera, kwa kuwa yeye aliwadhania ni wageni wanadamu na akaingiwa na masikitiko kwa kuwako kwao kwa kuwa ajua ubaya wa kitendo cha watu wake, na wao wakamwambia, «Usituogopee, kwani watu wako hawatatufikia. Na wala usiwe na masikitiko kwa kuwa tunakupasha habari kuwa sisi ni wenye kuwaangamiza wao. Sisi ni wenye kukuokoa wewe na hiyo adhabu itakayowashukia watu wako na ni wenye kuwaokoa watu wa nyumbani kwako pamoja nawe isipokuwa mke wako, kwani yeye ni mwenye kuangamia akiwa na wale wenye kuangamia katika watu wake |