Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 36 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿وَإِلَىٰ مَدۡيَنَ أَخَاهُمۡ شُعَيۡبٗا فَقَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱرۡجُواْ ٱلۡيَوۡمَ ٱلۡأٓخِرَ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ ﴾
[العَنكبُوت: 36]
﴿وإلى مدين أخاهم شعيبا فقال ياقوم اعبدوا الله وارجوا اليوم الآخر ولا﴾ [العَنكبُوت: 36]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tulimtumiliza, kwa watu wa Madyan, ndugu yao, Shu'ayb. Akawaambia, «Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu Peke Yake, na mumtakasie Ibada, kwani nyinyi hamuna Mola isipokuwa Yeye. Na kuweni na matarajio mema, kwa ibada mnazofanya, kupata malipo mazuri ya Siku ya Akhera, na msifanye uharibifu na maasia kwa wingi, na msijikite juu ya hayo. Lakini tubieni kwa Mwenyezi Mungu kwa makosa hayo na mrudi Kwake |