Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 48 - العَنكبُوت - Page - Juz 21
﴿وَمَا كُنتَ تَتۡلُواْ مِن قَبۡلِهِۦ مِن كِتَٰبٖ وَلَا تَخُطُّهُۥ بِيَمِينِكَۖ إِذٗا لَّٱرۡتَابَ ٱلۡمُبۡطِلُونَ ﴾
[العَنكبُوت: 48]
﴿وما كنت تتلو من قبله من كتاب ولا تخطه بيمينك إذا لارتاب﴾ [العَنكبُوت: 48]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa miujiza yako iliyo wazi, ewe Mtume, ni kuwa wewe hukusoma kitabu wala hukuandika herufi zozote kwa mkono wako wa kulia kabla ya hii Qur’ani kukuteremkia, na hali wao wanalijua hilo. Na lau ungalikuwa ni mwenye kusoma au kuandika kabla hujaletewa wahyi wangalilifanyia shaka hilo hao wapotofu na wangalisema, «Amejifunza hiyo (Qur’ani) au ameinakili kutoka kwenye vitabu vilivyotangulia.» |