Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 50 - العَنكبُوت - Page - Juz 21
﴿وَقَالُواْ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ ءَايَٰتٞ مِّن رَّبِّهِۦۚ قُلۡ إِنَّمَا ٱلۡأٓيَٰتُ عِندَ ٱللَّهِ وَإِنَّمَآ أَنَا۠ نَذِيرٞ مُّبِينٌ ﴾
[العَنكبُوت: 50]
﴿وقالوا لولا أنـزل عليه آيات من ربه قل إنما الآيات عند الله﴾ [العَنكبُوت: 50]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na washirikina walisema, «Si ateremshiwe Muammad dalili na hoja kutoka kwa Mola wake, kama vile ngamia wa Ṣāliḥ na fimbo ya Mūsā!» Waambie, «Jambo la miujiza hii liko kwa Mwenyezi Mungu, Akitaka Ataiteremsha na Akitaka Ataizuia. Na hakika ni kwamba mimi ni muonyaji, ninawatahadharisha na ukali wa adhabu Yake na mateso Yake, na ni mwenye kuwaonyesha njia ya haki na batili.» |