Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 60 - العَنكبُوت - Page - Juz 21
﴿وَكَأَيِّن مِّن دَآبَّةٖ لَّا تَحۡمِلُ رِزۡقَهَا ٱللَّهُ يَرۡزُقُهَا وَإِيَّاكُمۡۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ ﴾
[العَنكبُوت: 60]
﴿وكأين من دابة لا تحمل رزقها الله يرزقها وإياكم وهو السميع العليم﴾ [العَنكبُوت: 60]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ni viumbe vingapi vitambaavyo visivyojiwekea akiba ya chakula chao cha kesho, kama vile mwanadamu anavyofanya. Basi Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kuwa juu, Anaviruzuku kama Anavyowaruzuku nyinyi. Na Yeye ni Msikizi wa maneno yenu, ni Mjuzi wa vitendo vyenu na mawazo ya nyoyo zenu |