Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 63 - العَنكبُوت - Page - Juz 21
﴿وَلَئِن سَأَلۡتَهُم مَّن نَّزَّلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَحۡيَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ مِنۢ بَعۡدِ مَوۡتِهَا لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُۚ قُلِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡقِلُونَ ﴾
[العَنكبُوت: 63]
﴿ولئن سألتهم من نـزل من السماء ماء فأحيا به الأرض من بعد﴾ [العَنكبُوت: 63]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na ukiwauliza, ewe Mtume, hao washirikina, «Ni nani anayeteremsha maji kutoka mawinguni, yakaotesha mimea juu ya ardhi baada ya kuwa imekauka?» watakwambia huku wakikubali, «Mwenyezi Mungu Peke Yake Ndiye Anayeyateremsha hayo.» Sema, «Shukrani ni za Mwenyezi Mungu Aliyedhihirisha hoja yako kwao. Lakini wengi wao hawafahamu yanayowafaa wala yanayowadhuru, na lau waelewa hawangalimshirikisha Mwenyezi Mungu na Mwengine |