Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 68 - العَنكبُوت - Page - Juz 21
﴿وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِٱلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَهُۥٓۚ أَلَيۡسَ فِي جَهَنَّمَ مَثۡوٗى لِّلۡكَٰفِرِينَ ﴾
[العَنكبُوت: 68]
﴿ومن أظلم ممن افترى على الله كذبا أو كذب بالحق لما جاءه﴾ [العَنكبُوت: 68]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakuna yoyote aliye na udhalimu mkubwa kuliko yule aliyemkanusha Mwenyezi Mungu na akamnasibishia Mwenyezi Mungu upotevu alio nao na ubatilifu, au akaikanusha haki ambayo Mwenyezi Mungu Amemleta nayo Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Hakika ndani ya Moto ni makao ya aliyemkanusha Mwenyezi Mungu na akaukataa upweke Wake na akamkanusha Mtume Wake Muhammad,rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie |