Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 69 - العَنكبُوت - Page - Juz 21
﴿وَٱلَّذِينَ جَٰهَدُواْ فِينَا لَنَهۡدِيَنَّهُمۡ سُبُلَنَاۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَمَعَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ ﴾
[العَنكبُوت: 69]
﴿والذين جاهدوا فينا لنهدينهم سبلنا وإن الله لمع المحسنين﴾ [العَنكبُوت: 69]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Waumini waliopigana jihadi na maadui wa Mwenyezi Mungu, nafsi na Shetani na wakavumilia kwenye misukosuko na makero katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu Atawaongoa kwenye wema na kuwasimamisha imara juu ya njia iliyolingana sawa. Na yoyote ambaye sifa yake ni hii, basi yeye amejifanyia wema nafsi yake na amewafanyia wema wengine. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kuwa juu, Yupo pamoja na wale viumbe wake waliofanya wema, kwa kuwapa ushindi, kuwatilia nguvu, kuwahifadhi na kuwaongoza |