Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 106 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿يَوۡمَ تَبۡيَضُّ وُجُوهٞ وَتَسۡوَدُّ وُجُوهٞۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ٱسۡوَدَّتۡ وُجُوهُهُمۡ أَكَفَرۡتُم بَعۡدَ إِيمَٰنِكُمۡ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡفُرُونَ ﴾
[آل عِمران: 106]
﴿يوم تبيض وجوه وتسود وجوه فأما الذين اسودت وجوههم أكفرتم بعد إيمانكم﴾ [آل عِمران: 106]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Siku ya Kiyama zitakuwa nyeupe nyuso za watu wema ambao wamemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafuata amri Yake; na zitakuwa nyeusi nyuso za watu waovu kati ya wale waliomkanusha Mtume Wake na wakaasi amri Yake. Basi wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeusi wataambiwa kwa kulaumiwa, «Je, mumekufuru baada ya kuamini kwenu, mkachagua ukafiri mkaacha Imani? Basi ionjeni adhabu kwa sababu ya ukafiri wenu.» |