×

Wamepigwa na udhalili popote wanapo kutikana, isipo kuwa wakishika kamba ya Mwenyezi 3:112 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah al-‘Imran ⮕ (3:112) ayat 112 in Swahili

3:112 Surah al-‘Imran ayat 112 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 112 - آل عِمران - Page - Juz 4

﴿ضُرِبَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلذِّلَّةُ أَيۡنَ مَا ثُقِفُوٓاْ إِلَّا بِحَبۡلٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَحَبۡلٖ مِّنَ ٱلنَّاسِ وَبَآءُو بِغَضَبٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَضُرِبَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلۡمَسۡكَنَةُۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَانُواْ يَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَيَقۡتُلُونَ ٱلۡأَنۢبِيَآءَ بِغَيۡرِ حَقّٖۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَواْ وَّكَانُواْ يَعۡتَدُونَ ﴾
[آل عِمران: 112]

Wamepigwa na udhalili popote wanapo kutikana, isipo kuwa wakishika kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu. Na wakastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na wamepigwa na unyonge. Hayo ni kwa sababu walikuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakiwauwa Manabii pasina haki; hayo ni kwa sababu waliasi na walikuwa wakiruka mipaka

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ضربت عليهم الذلة أين ما ثقفوا إلا بحبل من الله وحبل من, باللغة السواحيلية

﴿ضربت عليهم الذلة أين ما ثقفوا إلا بحبل من الله وحبل من﴾ [آل عِمران: 112]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Amejaalia Mwenyezi Mungu utwevu na unyonge kuwa ni jambo lenye kuambatana nao Mayahudi na wala haliwaepuki. Kwa hivyo, wao daima ni madhalili wenye kudharauliwa popote waliopo, isipokuwa watakapokuwa na mafungamano na Mwenyezi Mungu na makubaliano na watu ambayo kwayo watajiwekea usalama wa nafsi zao na mali zao. Hayo ndiyo mapatano ya kujidhamini kwao na kujilazimisha kwao kufuata hukumu za Uislamu. Na wamerudi nyuma wakiwa wamepata hasira za Mwenyezi Mungu zilizowastahili. Na wamepigwa na unyonge na umasikini. Kwa hivyo, humuoni Myahudi isipokuwa utamkuta ameshukiwa na hofu na babaiko kwa kuwaogopa Waumini. Hilo ndilo Alilowajaalia Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kumkufuru kwao Mwenyezi Mungu, kukeuka kwao mipaka Yake na kuwaua kwao Manabii, kwa udhalimu na uonevu. Na hakuna lolote lililowafanya wao wawe majasiri wa kuyatenda haya isipokuwa ni kule kufanya kwao maasia na kukiuka kwao mipaka ya Mwenyezi Mungu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek