Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 130 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَأۡكُلُواْ ٱلرِّبَوٰٓاْ أَضۡعَٰفٗا مُّضَٰعَفَةٗۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ ﴾
[آل عِمران: 130]
﴿ياأيها الذين آمنوا لا تأكلوا الربا أضعافا مضاعفة واتقوا الله لعلكم تفلحون﴾ [آل عِمران: 130]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo, tahadharini na aina zote za riba na msichukue katika mkopo zaidi ya rasilmali zenu, hata kama ni kidogo. Basi itakuwaje iwapo ziada hiyo itaongezeka kila ufikapo muda wa kulipa deni? Na muogopeni Mwenyezi Mungu kwa kujilazimisha kufuata Sheria Zake ili mpate kufaulu duniani na Akhera |