×

Pale mlipo kuwa mkikimbia mbio wala hamumsikilizi yeyote, na Mtume anakuiteni, yuko 3:153 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah al-‘Imran ⮕ (3:153) ayat 153 in Swahili

3:153 Surah al-‘Imran ayat 153 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 153 - آل عِمران - Page - Juz 4

﴿۞ إِذۡ تُصۡعِدُونَ وَلَا تَلۡوُۥنَ عَلَىٰٓ أَحَدٖ وَٱلرَّسُولُ يَدۡعُوكُمۡ فِيٓ أُخۡرَىٰكُمۡ فَأَثَٰبَكُمۡ غَمَّۢا بِغَمّٖ لِّكَيۡلَا تَحۡزَنُواْ عَلَىٰ مَا فَاتَكُمۡ وَلَا مَآ أَصَٰبَكُمۡۗ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ ﴾
[آل عِمران: 153]

Pale mlipo kuwa mkikimbia mbio wala hamumsikilizi yeyote, na Mtume anakuiteni, yuko nyuma yenu. Mwenyezi Mungu akakupeni dhiki juu ya dhiki, ili msisikitike kwa yaliyo kukoseeni wala kwa yaliyo kusibuni. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إذ تصعدون ولا تلوون على أحد والرسول يدعوكم في أخراكم فأثابكم غما, باللغة السواحيلية

﴿إذ تصعدون ولا تلوون على أحد والرسول يدعوكم في أخراكم فأثابكم غما﴾ [آل عِمران: 153]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Kumbukeni, enyi maswahaba wa Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, hali zenu zilivyokuwa, mlipokuwa mnalipanda jabali mkiwakimbia maadui zenu, wala hamgeuki kumwangalia yoyote kwa sababu ya yale yaliyowafikia ya babaiko, kuogopa na fazaa. Na huku Mtume wa Mwenyezi Mungu , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, amekita kwenye uwanja wa vita, anawaita nyuma yenu kwa kuwaambia, «Njooni kwangu, enyi waja wa Mwenyezi Mungu,» hali ya kuwa nyinyi hamsikii wala hamuangalii. Hapo yakawa malipo yenu ni kupatwa na machungu, dhiki na kero. Aliyafanya hayo Mwenyezi Mungu ili msihuzunike kwa mliyoyakosa ya ushindi na ngawira wala yaliyowafikia ya kuingiwa na kicho na kushindwa. Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi wa matendo yenu yote; hakuna chochote katika hayo kinachofichika Kwake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek