×

Kisha baada ya dhiki alikuteremshieni utulivu - usingizi ambao ulifunika kundi moja 3:154 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah al-‘Imran ⮕ (3:154) ayat 154 in Swahili

3:154 Surah al-‘Imran ayat 154 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 154 - آل عِمران - Page - Juz 4

﴿ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيۡكُم مِّنۢ بَعۡدِ ٱلۡغَمِّ أَمَنَةٗ نُّعَاسٗا يَغۡشَىٰ طَآئِفَةٗ مِّنكُمۡۖ وَطَآئِفَةٞ قَدۡ أَهَمَّتۡهُمۡ أَنفُسُهُمۡ يَظُنُّونَ بِٱللَّهِ غَيۡرَ ٱلۡحَقِّ ظَنَّ ٱلۡجَٰهِلِيَّةِۖ يَقُولُونَ هَل لَّنَا مِنَ ٱلۡأَمۡرِ مِن شَيۡءٖۗ قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَمۡرَ كُلَّهُۥ لِلَّهِۗ يُخۡفُونَ فِيٓ أَنفُسِهِم مَّا لَا يُبۡدُونَ لَكَۖ يَقُولُونَ لَوۡ كَانَ لَنَا مِنَ ٱلۡأَمۡرِ شَيۡءٞ مَّا قُتِلۡنَا هَٰهُنَاۗ قُل لَّوۡ كُنتُمۡ فِي بُيُوتِكُمۡ لَبَرَزَ ٱلَّذِينَ كُتِبَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقَتۡلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمۡۖ وَلِيَبۡتَلِيَ ٱللَّهُ مَا فِي صُدُورِكُمۡ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمۡۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ ﴾
[آل عِمران: 154]

Kisha baada ya dhiki alikuteremshieni utulivu - usingizi ambao ulifunika kundi moja kati yenu. Na kundi jengine nafsi zao ziliwashughulisha hata wakamdhania Mwenyezi Mungu dhana isiyo kuwa ya haki, dhana ya kijinga. Wakisema: Hivyo tuna lolote sisi katika jambo hili? Sema: Mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Wanaficha katika nafsi zao wasiyo kubainishia. Wanasema: Lau ingelikuwa tuna lolote katika jambo hili tusinge uliwa hapa. Sema: Hata mngeli kuwa majumbani mwenu, basi wangeli toka walio andikiwa kufa, wakenda mahali pao pa kuangukia wafe. (Haya ni hivyo) ili Mwenyezi Mungu ayajaribu yaliyomo vifuani mwenu, na asafishe yaliyomo nyoyoni mwenu. Na Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo vifuani

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ثم أنـزل عليكم من بعد الغم أمنة نعاسا يغشى طائفة منكم وطائفة, باللغة السواحيلية

﴿ثم أنـزل عليكم من بعد الغم أمنة نعاسا يغشى طائفة منكم وطائفة﴾ [آل عِمران: 154]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Kisha ikawa ni katika rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waumini waliomtakasia nia kwamba Aliingiza kwenye nyoyo zao , baada ya kero na usumbufu uliowafika, utulivu na Imani thabiti kuhusu ahadi ya Mwenyezi Mungu kwao. Miongoni mwa alama za utulivu huo ni usingizi uliolifinika kundi katika wao, nalo ni lile la wale waliokuwa na ikhlasi na yakini kwa Mola wao. Na kundi lingine ilikuwa hamu ya watu wake ni kuziokoa nafsi zao; azma yao ilikuwa dhaifu, wakashughulishwa na nafsi zao na wakawa na dhana mbaya kwa Mola wao, kwa Dini Yake na kwa Mtume Wake.Wakadhani kwamba Mwenyezi Mungu Hatalitimiza jambo la Mtume Wake na kwamba Uislamu hautasimama ukaimarika. Kwa hivyo, utawaona ni wenye majuto juu ya kutoka kwao. Na huwa wakiambiana wao kwa wao, «Je tulikuwa na chaguo lolote katika kutoka kwetu kwenda kupigana?» Waambie, ewe Mtume, «Mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Yeye Ndiye Aliyepanga kutoka kwenu na (Ndiye Aliyepanga yale) yaliyowafikia.» Nao wanayaficha katika nafsi zao wasiyoyadhihirisha kwako ya majuto juu ya kutoka kwao kwenda mapiganoni. Huwa wakisema, «Lau kama tungalikuwa na hiyari japo ndogo, hatungeuawa hapa.» Waambie, «Ajali ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Hata kama mlikuwa majumbani mwenu, na Mwenyezi Mungu Akakadiria mufe, wangalitoka wale ambao Mwenyezi Mungu Amewakadiria mauti, kwenda pale watakapouawa.» Na Hakuyafanya hayo Mwenyezi Mungu isipokuwa ni kuwapa nyinyi mtihani juu ya yaliyomo ndani ya vifua vyenu ya shaka na unafiki na ili Ampambanue mwema na maovu na lipate kudhihirika kwa watu jambo la Muumini na lile la mnafiki, la maneno na vitendo. Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi wa yaliyomo kwenye nyoyo za viumbe Wake. Hakuna chochote, katika mambo yao, kinachofichika Kwake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek