Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 188 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿لَا تَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ يَفۡرَحُونَ بِمَآ أَتَواْ وَّيُحِبُّونَ أَن يُحۡمَدُواْ بِمَا لَمۡ يَفۡعَلُواْ فَلَا تَحۡسَبَنَّهُم بِمَفَازَةٖ مِّنَ ٱلۡعَذَابِۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ ﴾
[آل عِمران: 188]
﴿لا تحسبن الذين يفرحون بما أتوا ويحبون أن يحمدوا بما لم يفعلوا﴾ [آل عِمران: 188]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wala msiwadhanie wale wanaofurahia matendo maovu waliyoyafanya, kama Mayahudi, wanafiki na wengineo, na wakawa wanapenda kuwa watu wawataje vizuri kwa mambo ambayo hawakuyafanya, basi msiwadhanie wao kuwa ni wenye kuokoka na adhabu ya Mwenyezi Mungu duniani. Na watakuwa na adhabu iumizayo kesho Akhera. Katika haya kuna onyo kali kwa kila mwenye kutenda kitendo kiovu na kukifurahia na kwa kila mwenye kujigamba kwa ambacho hakukifanya ili watu wamsifu na kumshukuru |