Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 18 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿شَهِدَ ٱللَّهُ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَأُوْلُواْ ٱلۡعِلۡمِ قَآئِمَۢا بِٱلۡقِسۡطِۚ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ ﴾
[آل عِمران: 18]
﴿شهد الله أنه لا إله إلا هو والملائكة وأولو العلم قائما بالقسط﴾ [آل عِمران: 18]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Ameshuhudia kuwa Yeye Ndiye Aliyepwekeka kwa uungu. Na Ameambatanisha ushahidi wake na ule wa Malaika na watu wa elimu juu ya kitu kitukufu zaidi chenye kushuhudiwa, nacho ni Tawhīd umoja Wake Aliyetukuka na kusimamia Kwake haki na uadilifu. Hapana Mola isipokuwa Yeye, Aliye Mshindi Ambaye hakuna kitu Atakacho kiwe kikakataa kuwa, Mwenye hekima katikia maneno Yake na vitendo Vyake |