Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 196 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿لَا يَغُرَّنَّكَ تَقَلُّبُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي ٱلۡبِلَٰدِ ﴾
[آل عِمران: 196]
﴿لا يغرنك تقلب الذين كفروا في البلاد﴾ [آل عِمران: 196]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Usihadaike, ewe Mtume, kwa yale waliyonayo wenye kumkufuru Mwenyezi Mungu, ya ukunjufu wa riziki, hali nzuri ya maisha na kuhama kwao kutoka mahali kwenda pengine kwa ajili ya biashara na kutaka faida na mali. Kwa muda mchache, yote hayo yatawaondokea na watakuwa ni wenye kufungika na kuwekwa dhamana kwa vitendo vyao viovu |