×

Hakika miongoni mwa Watu wa Kitabu wapo wanao muamini Mwenyezi Mungu na 3:199 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah al-‘Imran ⮕ (3:199) ayat 199 in Swahili

3:199 Surah al-‘Imran ayat 199 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 199 - آل عِمران - Page - Juz 4

﴿وَإِنَّ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَمَن يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكُمۡ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِمۡ خَٰشِعِينَ لِلَّهِ لَا يَشۡتَرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ ثَمَنٗا قَلِيلًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ ﴾
[آل عِمران: 199]

Hakika miongoni mwa Watu wa Kitabu wapo wanao muamini Mwenyezi Mungu na yaliyo teremshwa kwenu na yaliyo teremshwa kwao, wakimnyenyekea Mwenyezi Mungu. Hawabadili Aya za Mwenyezi Mungu kwa thamani duni. Hao wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وإن من أهل الكتاب لمن يؤمن بالله وما أنـزل إليكم وما أنـزل, باللغة السواحيلية

﴿وإن من أهل الكتاب لمن يؤمن بالله وما أنـزل إليكم وما أنـزل﴾ [آل عِمران: 199]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Baadhi ya waliopewa vitabu wanamuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni Mola Mmoja na Mungu Mwenye kuabudiwa, wanaiamini Qur’ani mliyoteremshiwa nyinyi na Taurati na Injili walizoteremshiwa wao, hali ya kumdhalilikia Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea. Hawazibadilishi aya za Mwenyezi Mungu kwa thamani ndogo ya takataka za duniani wala hawayafichi Aliyoyataremsha Mwenyezi Mungu na wala hawayapotoshi kama wanavyofanya wengineo miongoni mwa waliopewa Vitabu. Hao watapata thawabu kubwa mbele ya Mola wao Siku ya kukutana Naye, na watapewa malipo yao kamili, bila ya kupunguzwa. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu. Hakumshindi Yeye kuyadhibiti matendo yao na kuwahesabu wao kwayo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek