Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 198 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿لَٰكِنِ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ رَبَّهُمۡ لَهُمۡ جَنَّٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا نُزُلٗا مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِۗ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ خَيۡرٞ لِّلۡأَبۡرَارِ ﴾
[آل عِمران: 198]
﴿لكن الذين اتقوا ربهم لهم جنات تجري من تحتها الأنهار خالدين فيها﴾ [آل عِمران: 198]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Lakini wale waliomuogopa Mola wao , wakazifuata amri Zake na wakajiepusha na makatazo Yake, Mwenyezi Mungu Amewaandalia mabustani ya Pepo ambayo mito inapita chini ya majumba yake ya fahari na miti yake. Mabustani hayo yatakuwa ni makazi yao ya kudumu; hawatatoka humo. Na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni makubwa zaidi na bora zaidi kwa watiifu kuliko yale ya starehe za ulimwengu ambazo hao waliokufuru wanatanga huku na kule kwa kuzitafuta |