Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 27 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿تُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِي ٱلنَّهَارِ وَتُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِي ٱلَّيۡلِۖ وَتُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَتُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتَ مِنَ ٱلۡحَيِّۖ وَتَرۡزُقُ مَن تَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٖ ﴾
[آل عِمران: 27]
﴿تولج الليل في النهار وتولج النهار في الليل وتخرج الحي من الميت﴾ [آل عِمران: 27]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Na miongoni mwa dalili za uwezo Wako, ni kuwa Wewe Unautia usiku ndani ya mchana, na Unautia mchana ndani ya uslku, huu ukarefuka na ule ukafupika. Na Unatoa chenye uhai kutoka kwa kilichokufa kisichokuwa na uhai, kama kutoa mazao kutokana na mbegu na kama kumtoa Muumini kutoka kwa kafiri. Na Unatoa kilichokufa kutoka kwa chenye uhai, kama kutoa yai kwenye kuku. Na Unamruzuku Unayemtaka katika waja Wako bila hesabu.» |