Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 59 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ ٱللَّهِ كَمَثَلِ ءَادَمَۖ خَلَقَهُۥ مِن تُرَابٖ ثُمَّ قَالَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ ﴾
[آل عِمران: 59]
﴿إن مثل عيسى عند الله كمثل آدم خلقه من تراب ثم قال﴾ [آل عِمران: 59]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika mfano wa Mwenyezi Mungu kumuumba 'Īlsa, bila ya baba, ni kama mfano wa Mwenyezi Mungu kumuumba Adam, bila ya baba wala mama. Mwenyezi Mungu Alimuumba kutokana na mchanga wa ardhi kisha Akamwabia, «kuwa kiumbe», akawa. Basi madai ya uungu wa 'Īsā kwa kuwa aliumbwa bila ya baba, ni madai ya urongo. Ādam, amani imshukie, aliumbwa bila ya baba wala mama, na wote wamekubaliana kwamba yeye ni mja miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu |