Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 61 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿فَمَنۡ حَآجَّكَ فِيهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ فَقُلۡ تَعَالَوۡاْ نَدۡعُ أَبۡنَآءَنَا وَأَبۡنَآءَكُمۡ وَنِسَآءَنَا وَنِسَآءَكُمۡ وَأَنفُسَنَا وَأَنفُسَكُمۡ ثُمَّ نَبۡتَهِلۡ فَنَجۡعَل لَّعۡنَتَ ٱللَّهِ عَلَى ٱلۡكَٰذِبِينَ ﴾
[آل عِمران: 61]
﴿فمن حاجك فيه من بعد ما جاءك من العلم فقل تعالوا ندع﴾ [آل عِمران: 61]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi yoyote mwenye kujadiliana nawe , ewe Mtume, kuhusu Al-Masīḥ ‘Īsā mwana wa Maryam, baada ya ujuzi uliokufikia juu ya ‘Īsā, amani imshukie, waambie, «Njooni tuwahudhurishe watoto wetu wa kiume na watoto wenu wa kiume, wanawake wetu na wanawake wenu na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuelekee kwa Mwenyezi Mungu kwa kumuomba Ayashukishe mateso Yake na laana Yake juu ya warongo katika maneno yao, wenye kukamaa katika upotofu wao.» |