Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 76 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿بَلَىٰۚ مَنۡ أَوۡفَىٰ بِعَهۡدِهِۦ وَٱتَّقَىٰ فَإِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُتَّقِينَ ﴾
[آل عِمران: 76]
﴿بلى من أوفى بعهده واتقى فإن الله يحب المتقين﴾ [آل عِمران: 76]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mambo si kama vile walivyodai hawa warongo. Mchaji-Mungu kikweli ni yule aliyetekeleza ahadi aliyomuahidi Mwenyezi Mungu ya kutekeleza amana na kumuamini Yeye na Mitume Wake na akajilazimisha kufuata uongofu Wake na Sharia Yake na akamuogopa Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka, kwa kufuata Aliyoamrisha na kujiepusha na Aliyokataza. Na Mwenyezi Mungu Anawapenda wachamungu wenye kujikinga na ushirikina na maasia |