Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 79 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤۡتِيَهُ ٱللَّهُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحُكۡمَ وَٱلنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُواْ عِبَادٗا لِّي مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِن كُونُواْ رَبَّٰنِيِّـۧنَ بِمَا كُنتُمۡ تُعَلِّمُونَ ٱلۡكِتَٰبَ وَبِمَا كُنتُمۡ تَدۡرُسُونَ ﴾
[آل عِمران: 79]
﴿ما كان لبشر أن يؤتيه الله الكتاب والحكم والنبوة ثم يقول للناس﴾ [آل عِمران: 79]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Haitakiwi kwa binadamu yoyote ateremshiwe kitabu na Mwenyezi Mungu chenye kutoa uamuzi kwa viumbe Wake na achaguliwe kuwa ni Nabii, kisha awaambie watu, «Niabuduni mimi badala ya Mwenyezi Mungu.» Lakini atasema, «Kuweni ni watu wa busara, wenye kuelewa na wajuzi wa wahyi wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, mliokuwa mkiwafundisha wengine na mnaousoma kwa kuuhifadhi, kuujua na kuuelewa..» |