Quran with Swahili translation - Surah Ar-Rum ayat 58 - الرُّوم - Page - Juz 21
﴿وَلَقَدۡ ضَرَبۡنَا لِلنَّاسِ فِي هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ مِن كُلِّ مَثَلٖۚ وَلَئِن جِئۡتَهُم بِـَٔايَةٖ لَّيَقُولَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا مُبۡطِلُونَ ﴾
[الرُّوم: 58]
﴿ولقد ضربنا للناس في هذا القرآن من كل مثل ولئن جئتهم بآية﴾ [الرُّوم: 58]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika tuliwafafanulia watu, katika hii Qur’ani, kila mfano ili kuwasimamishia hoja na kuthibitisha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja, Aliyetukuka na kuwa juu. Na lau ungaliwajia na hoja yoyote yenye kuonyesha ukweli wako, wale waliokukanusha wangalisema kukwambia, «Hamkuwa nyinyi, ewe Mtume na wafuasi wako, isipokuwa ni warongo katika yale mambo mnayotuletea.» |