Quran with Swahili translation - Surah Luqman ayat 15 - لُقمَان - Page - Juz 21
﴿وَإِن جَٰهَدَاكَ عَلَىٰٓ أَن تُشۡرِكَ بِي مَا لَيۡسَ لَكَ بِهِۦ عِلۡمٞ فَلَا تُطِعۡهُمَاۖ وَصَاحِبۡهُمَا فِي ٱلدُّنۡيَا مَعۡرُوفٗاۖ وَٱتَّبِعۡ سَبِيلَ مَنۡ أَنَابَ إِلَيَّۚ ثُمَّ إِلَيَّ مَرۡجِعُكُمۡ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ ﴾
[لُقمَان: 15]
﴿وإن جاهداك على أن تشرك بي ما ليس لك به علم فلا﴾ [لُقمَان: 15]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Na wakikusukuma kwa bidii wazazi wako wawili, ewe mtoto mwema, ili unishirikishe mimi na mwingine katika kuniabudu katika kitu ambacho huna ujuzi nacho, au wakakuamuru ufanye jambo miongoni mwa mambo ya kumuasi Mwenyezi Mungu basi usiwatii, kwani hakuna kutiiwa kiumbe kwa kuasiwa Muumba. Na suhubiana nao ulimwenguni kwa wema katika mambo mema yasiyo na madhambi. Na ufuate, ewe mwana mwenye Imani, njia ya aliyetubu kutokana na dhambi zake, akarudi kwangu na akamuamini Mtume wangu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Kisha ni kwangu mimi marejeo yenu, niwape habari ya yale mliokuwa mkiyafanya duniani na nimlipe kila mtenda kwa matendo yake |