Quran with Swahili translation - Surah Luqman ayat 34 - لُقمَان - Page - Juz 21
﴿إِنَّ ٱللَّهَ عِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلسَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ ٱلۡغَيۡثَ وَيَعۡلَمُ مَا فِي ٱلۡأَرۡحَامِۖ وَمَا تَدۡرِي نَفۡسٞ مَّاذَا تَكۡسِبُ غَدٗاۖ وَمَا تَدۡرِي نَفۡسُۢ بِأَيِّ أَرۡضٖ تَمُوتُۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرُۢ ﴾
[لُقمَان: 34]
﴿إن الله عنده علم الساعة وينـزل الغيث ويعلم ما في الأرحام وما﴾ [لُقمَان: 34]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Anajuwa ni lini Kiyama kitasimama. Na Yeye Ndiye Anayeteremsha mvua kutoka mawinguni, hakuna awezae hilo yoyote isipokuwa Yeye. Na Anajua vilivyomo ndani ya vizazi vya wanawake. Na Anajua kitakachotendwa na kila mtu wakati ujao. Na hakuna nafsi inayojua itakufa wapi. Ni Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Peke Yake Ndiye Anayehusika kwa kujua hayo yote. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi, Ameyazunguka mambo ya nje na ya ndani, hakuna chochote katika hayo kinachofichamana Kwake |