Quran with Swahili translation - Surah As-Sajdah ayat 11 - السَّجدة - Page - Juz 21
﴿۞ قُلۡ يَتَوَفَّىٰكُم مَّلَكُ ٱلۡمَوۡتِ ٱلَّذِي وُكِّلَ بِكُمۡ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمۡ تُرۡجَعُونَ ﴾
[السَّجدة: 11]
﴿قل يتوفاكم ملك الموت الذي وكل بكم ثم إلى ربكم ترجعون﴾ [السَّجدة: 11]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Atakayewafisha nyinyi ni Malaika wa kifo aliyewakilishwa kwenu, atakayezichukua roho zenu utakapokoma muda wenu wa kuishi, na hamtachelewa hata nukta moja, kisha mtarudishwa kwa Mola wenu, Awalipe kwa matendo yenu, yakiwa ni mema Awalipe wema na yakiwa maovu Awalipe uovu |