Quran with Swahili translation - Surah As-Sajdah ayat 30 - السَّجدة - Page - Juz 21
﴿فَأَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ وَٱنتَظِرۡ إِنَّهُم مُّنتَظِرُونَ ﴾
[السَّجدة: 30]
﴿فأعرض عنهم وانتظر إنهم منتظرون﴾ [السَّجدة: 30]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi wape mgongo, ewe Mtume, hawa washirikina, na usiujali ukanushaji wao, na ungojee vile Mwenyezi Mungu Atawafanya. Hakika wao ni wenye kungojea na kutaraji mpatikane na ubaya. Basi Mwenyezi Mungu Atawapa hizaya na Atawadhalilisha na Akupe ushindi juu yao. Na Mwenyezi Mungu Ashalifanya hilo, sifa njema ni Zake na wema ni Wake |