Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 13 - الأحزَاب - Page - Juz 21
﴿وَإِذۡ قَالَت طَّآئِفَةٞ مِّنۡهُمۡ يَٰٓأَهۡلَ يَثۡرِبَ لَا مُقَامَ لَكُمۡ فَٱرۡجِعُواْۚ وَيَسۡتَـٔۡذِنُ فَرِيقٞ مِّنۡهُمُ ٱلنَّبِيَّ يَقُولُونَ إِنَّ بُيُوتَنَا عَوۡرَةٞ وَمَا هِيَ بِعَوۡرَةٍۖ إِن يُرِيدُونَ إِلَّا فِرَارٗا ﴾
[الأحزَاب: 13]
﴿وإذ قالت طائفة منهم ياأهل يثرب لا مقام لكم فارجعوا ويستأذن فريق﴾ [الأحزَاب: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbuka, ewe Nabii, neno la kipote cha wanafiki wakiwaita Waumini miongoni mwa watu wa Madina, «Enyi watu wa Yathrib (nalo ni jina la zamani la Madina), ‘Msikae kwenye vita ambavyo mtashindwa, rudini majumbani mwenu ndani ya Madina’» Na pote lingine la wanafiki linamuomba ruhusa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kurudi majumbani mwao kwa kisingizio kuwa hayako imara, na kwa hivyo wanayaogopea, na ukweli ni kwamba hayo si hivyo, na lengo lao halikuwa isipokuwa ni kukimbia vita |