Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 19 - الأحزَاب - Page - Juz 21
﴿أَشِحَّةً عَلَيۡكُمۡۖ فَإِذَا جَآءَ ٱلۡخَوۡفُ رَأَيۡتَهُمۡ يَنظُرُونَ إِلَيۡكَ تَدُورُ أَعۡيُنُهُمۡ كَٱلَّذِي يُغۡشَىٰ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡمَوۡتِۖ فَإِذَا ذَهَبَ ٱلۡخَوۡفُ سَلَقُوكُم بِأَلۡسِنَةٍ حِدَادٍ أَشِحَّةً عَلَى ٱلۡخَيۡرِۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَمۡ يُؤۡمِنُواْ فَأَحۡبَطَ ٱللَّهُ أَعۡمَٰلَهُمۡۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٗا ﴾
[الأحزَاب: 19]
﴿أشحة عليكم فإذا جاء الخوف رأيتهم ينظرون إليك تدور أعينهم كالذي يغشى﴾ [الأحزَاب: 19]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wanawafanyia nyinyi, enyi Waumini, ugumu wa mali, nafsi, juhudi na mapenzi kwa uadui na chuki walizonazo ndani ya nafsi zao, kwa kupenda kuishi na kuogopa kufa. Na vita vikisimama huwa wakiogopa kuangamia, na utawaona wanakuangalia, macho yao yanazunguka kwa kuwa akili zao zimeondoka kwa kuogopa na kukimbia kuuawa, kama vile macho ya mtu aliyekaribia kufa yanavyozunguka. Na vita vinapomalizika na hofu kuondoka wanawarushia nyinyi matamshi makali yenye kukera. Na utawakuta wao, zinapogawiwa ngawira, ni wachoyo na ni mahasidi. Hao hawakuamini kwa nyoyo zao ndipo Mwenyezi Mungu Akawaondolea thawabu za matendo yao, na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi |