Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 22 - الأحزَاب - Page - Juz 21
﴿وَلَمَّا رَءَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلۡأَحۡزَابَ قَالُواْ هَٰذَا مَا وَعَدَنَا ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَصَدَقَ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥۚ وَمَا زَادَهُمۡ إِلَّآ إِيمَٰنٗا وَتَسۡلِيمٗا ﴾
[الأحزَاب: 22]
﴿ولما رأى المؤمنون الأحزاب قالوا هذا ما وعدنا الله ورسوله وصدق الله﴾ [الأحزَاب: 22]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Waumini walipoyashuhudia mapote ya watu waliojikusanya pambizoni mwa mji wa Madina na wakauzunguka, walikumbuka kwamba ahadi ya ushindi imekaribia na wakasema, «Haya ndiyo yale Aiyotuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ya maonjo, shida na (kisha) ushindi. Mwenyezi Mungu Alitekeleza ahadi Yake na Mtume Wake alisema kweli katika bishara njema aliyoitoa. Na hakukuwaongezea kule kuyatazama yale mapote isipokuwa kumuamini Mwenyezi Mungu na kujisalimisha na uamuzi Wake na kufuata amri Yake |