Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 23 - الأحزَاب - Page - Juz 21
﴿مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ رِجَالٞ صَدَقُواْ مَا عَٰهَدُواْ ٱللَّهَ عَلَيۡهِۖ فَمِنۡهُم مَّن قَضَىٰ نَحۡبَهُۥ وَمِنۡهُم مَّن يَنتَظِرُۖ وَمَا بَدَّلُواْ تَبۡدِيلٗا ﴾
[الأحزَاب: 23]
﴿من المؤمنين رجال صدقوا ما عاهدوا الله عليه فمنهم من قضى نحبه﴾ [الأحزَاب: 23]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Miongoni mwa Waumini kuna wanaume waliotekeleza ahadi zao walizomuahidi Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na wakasubiri juu ya shida, madhara na wakati wa vita. Kati yao kuna aliyetekeleza nadhiri akafa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu au akafa juu ya ukweli na utekelezaji ahadi, na kati yao kuna anayengojea mojawapo ya mema mawili, ushindi au kufa shahidi, na hawakuigeuza ahadi ya Mwenyezi Mungu wala hawakuitangua wala hawakuibadilisha kama vile wanafiki walivyogeuza |