×

Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake 33:6 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Ahzab ⮕ (33:6) ayat 6 in Swahili

33:6 Surah Al-Ahzab ayat 6 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 6 - الأحزَاب - Page - Juz 21

﴿ٱلنَّبِيُّ أَوۡلَىٰ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ مِنۡ أَنفُسِهِمۡۖ وَأَزۡوَٰجُهُۥٓ أُمَّهَٰتُهُمۡۗ وَأُوْلُواْ ٱلۡأَرۡحَامِ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلَىٰ بِبَعۡضٖ فِي كِتَٰبِ ٱللَّهِ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُهَٰجِرِينَ إِلَّآ أَن تَفۡعَلُوٓاْ إِلَىٰٓ أَوۡلِيَآئِكُم مَّعۡرُوفٗاۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِي ٱلۡكِتَٰبِ مَسۡطُورٗا ﴾
[الأحزَاب: 6]

Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao. Na jamaa ni karibu wao kwa wao katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuliko Waumini wengine na Wahamiaji. Ila muwe mnawafanyia wema marafiki zenu. Haya yamekwisha andikwa Kitabuni

❮ Previous Next ❯

ترجمة: النبي أولى بالمؤمنين من أنفسهم وأزواجه أمهاتهم وأولو الأرحام بعضهم أولى ببعض, باللغة السواحيلية

﴿النبي أولى بالمؤمنين من أنفسهم وأزواجه أمهاتهم وأولو الأرحام بعضهم أولى ببعض﴾ [الأحزَاب: 6]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ni bora kwa Waumini na ni karibu na wao zaidi kuliko nafsi zao katika mambo ya dini na dunia. Na heshima ya wake za Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa ummah wake, kama vile heshima ya mama zao, haifai kuwaoa wake za Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, baada yake. Na wenye ujamaa wa ukaribu, miongoni mwa Waislamu, baadhi yao wana haki zaidi ya kuwarithi wengine katika hukumu ya Mwenyezi Mungu na sheria Yake kuliko kurithi kwa (misingi ya) Imani na uhamiaji. (Waislamu hapo mwanzo wa Uislamu walikuwa wakirithiana kwa misingi ya hijrah (uhamiaji) na Imani au Dini na si kwa kizazi, kisha hilo likaondolewa kwa aya ya urathi), isipokuwa iwapo nyinyi, enyi Waislamu, mtawafanyia wema kwa kuwahami, kuwafanyia wema, kuwaunga na kuwaachia wasia wa kuwafaidisha. Hukumu hii iliyotajwa imekadiriwa, imeandikwa kwenye Ubao uliyohifadhiwa, basi ni lazima kwenu muifuate kivitendo. Ndani ya aya hii pana ulazima wa kuwa Mtume, rehema na amani zimshukie, awe ni mwenye kupendwa zaidi na mja kuliko nafsi yake, na ulazima wa kumfuata yeye kikamilifu. Na ndani yake pana ulazima wa kuwaheshimu mama za Waumini, wake za Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kwamba mwenye kuwatukana atarudi na hasara
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek