Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 5 - الأحزَاب - Page - Juz 21
﴿ٱدۡعُوهُمۡ لِأٓبَآئِهِمۡ هُوَ أَقۡسَطُ عِندَ ٱللَّهِۚ فَإِن لَّمۡ تَعۡلَمُوٓاْ ءَابَآءَهُمۡ فَإِخۡوَٰنُكُمۡ فِي ٱلدِّينِ وَمَوَٰلِيكُمۡۚ وَلَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٞ فِيمَآ أَخۡطَأۡتُم بِهِۦ وَلَٰكِن مَّا تَعَمَّدَتۡ قُلُوبُكُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمًا ﴾
[الأحزَاب: 5]
﴿ادعوهم لآبائهم هو أقسط عند الله فإن لم تعلموا آباءهم فإخوانكم في﴾ [الأحزَاب: 5]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wale mnaodai kuwa ni wana wenu wanasibisheni na baba zao, hilo ni jambo la uadilifu zaidi na la sawa zaidi kwa Mwenyezi Mungu. Mkiwa hamuwajui baba zao wa kihakika, basi hapo waiteni kwa undugu wa Dini ambayo inawakusanya nyinyi na wao, kwani wao ni ndugu zenu katika Dini na pia ni marafiki zenu. Na nyinyi hamna dhambi kwa makosa mliyoyafanya bila kukusudia, lakini Mwenyezi Mungu Atawapatiliza mkifanya hilo kwa kusudi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha kwa aliokosea, ni Mwingi wa rehema kwa mwenye kutubia dhambi Zake |