Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 68 - الأحزَاب - Page - Juz 22
﴿رَبَّنَآ ءَاتِهِمۡ ضِعۡفَيۡنِ مِنَ ٱلۡعَذَابِ وَٱلۡعَنۡهُمۡ لَعۡنٗا كَبِيرٗا ﴾
[الأحزَاب: 68]
﴿ربنا آتهم ضعفين من العذاب والعنهم لعنا كبيرا﴾ [الأحزَاب: 68]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mola wetu! Waadhibu Motoni mara mbili zaidi ya adhabu unayotuadhibu kwayo, na uwafukuze kutoka kwenye rehema mafukuzo makali.» Katika hii pana dalili ya kwamba kumtii asiyekuwa Mwenyezi Mungu katika kuenda kinyume na amri Yake na amri ya Mtume Wake, kunapasisha kupata hasira za Mwenyezi Mungu na mateso Yake, na kwamba mfuasi na mfuatwa watashirikiana kwenye adhabu. Basi ajihadhari na hilo Muislamu |