Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 69 - الأحزَاب - Page - Juz 22
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ ءَاذَوۡاْ مُوسَىٰ فَبَرَّأَهُ ٱللَّهُ مِمَّا قَالُواْۚ وَكَانَ عِندَ ٱللَّهِ وَجِيهٗا ﴾
[الأحزَاب: 69]
﴿ياأيها الذين آمنوا لا تكونوا كالذين آذوا موسى فبرأه الله مما قالوا﴾ [الأحزَاب: 69]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo, msimkere Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa maneno wala kwa vitendo, wala msiwe mfano wa wale waliomkera Nabii wa Mwenyezi Mungu Mūsā, Mwenyezi Mungu Akamuepusha na kile walichokisema cha urongo na uzushi, na yeye alikuwa kwa Mwenyezi Mungu ni mwenye cheo kikubwa na utukufu |