Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 9 - الأحزَاب - Page - Juz 21
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ جَآءَتۡكُمۡ جُنُودٞ فَأَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ رِيحٗا وَجُنُودٗا لَّمۡ تَرَوۡهَاۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرًا ﴾
[الأحزَاب: 9]
﴿ياأيها الذين آمنوا اذكروا نعمة الله عليكم إذ جاءتكم جنود فأرسلنا عليهم﴾ [الأحزَاب: 9]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi Waumini! Ikumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Aliyowaneemesha nyinyi katika Madina siku ya vita vya Makundi (Aḥzāb), navyo ndivyo vita vya Shimo (Khandaq), walipojikusanya dhidi yenu washirikina kutoka nje ya Madina, na Mayahudi na wanafiki wakiwa ndani ya Madina na pambizoni mwake, wakawaviringa nyinyi, hapo tukayatumia yale makundi upepo mkali uliong’oa mahema yao na kuvirusha vyungu vyao, na tukawatumia Malaika kutoka mbinguni msiowaona, hapo basi nyoyo zao zikaingia kicho. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mnayoyatenda, hakuna chochote kinachofichamana kwake katika hayo |