Quran with Swahili translation - Surah Saba’ ayat 24 - سَبإ - Page - Juz 22
﴿۞ قُلۡ مَن يَرۡزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ قُلِ ٱللَّهُۖ وَإِنَّآ أَوۡ إِيَّاكُمۡ لَعَلَىٰ هُدًى أَوۡ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ ﴾
[سَبإ: 24]
﴿قل من يرزقكم من السموات والأرض قل الله وإنا أو إياكم لعلى﴾ [سَبإ: 24]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina, «Ni nani anayewaruzuku kwa mvua kutoka mbinguni, na kwa mimea na madini na vinginevyo kutoka ardhini?» Hivyo basi hawana budi kukubali kuwa Yeye ni Mwenyezi Mungu. Na iwapo hawatakubali hilo, waambie, «Mwenyezi Mungu Ndiye Mwingi wa kuruzuku, na kwa hakika mojawapo wa mapote mawili, kati ya sisi na nyinyi, limejikita kwenye uongofu au limevama kwenye upotevu ulio wazi.» |