Quran with Swahili translation - Surah Saba’ ayat 30 - سَبإ - Page - Juz 22
﴿قُل لَّكُم مِّيعَادُ يَوۡمٖ لَّا تَسۡتَـٔۡخِرُونَ عَنۡهُ سَاعَةٗ وَلَا تَسۡتَقۡدِمُونَ ﴾
[سَبإ: 30]
﴿قل لكم ميعاد يوم لا تستأخرون عنه ساعة ولا تستقدمون﴾ [سَبإ: 30]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Waamnbie, ewe Mtume, «Nyinyi muna maagano ambayo hapana budi yatawajia, nayo ni maagano ya Siku ya Kiyama, hamtachelewa nayo hata muda mchache wa kupata kutubia, na wala hamtatangulia mbele yake mkaadhibiwa hata kwa muda mchache. Basi jihadharini na Siku hiyo na jitayarisheni kwa vifaa vyake.» |