Quran with Swahili translation - Surah Saba’ ayat 31 - سَبإ - Page - Juz 22
﴿وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَن نُّؤۡمِنَ بِهَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ وَلَا بِٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِۗ وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذِ ٱلظَّٰلِمُونَ مَوۡقُوفُونَ عِندَ رَبِّهِمۡ يَرۡجِعُ بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٍ ٱلۡقَوۡلَ يَقُولُ ٱلَّذِينَ ٱسۡتُضۡعِفُواْ لِلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُواْ لَوۡلَآ أَنتُمۡ لَكُنَّا مُؤۡمِنِينَ ﴾
[سَبإ: 31]
﴿وقال الذين كفروا لن نؤمن بهذا القرآن ولا بالذي بين يديه ولو﴾ [سَبإ: 31]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na waliokanusha walisema, «Hatutaiamini hii Qur’ani wala vile vilivyoitangulia, kina Taurati, Injili na Zaburi.» Kwa hakika washakanusha vitabu vyote vya Mwenyezi Mungu. Na lau utaona pindi madhalimu wamefungwa mbele ya Mola wao ili wahesabiwe, huku wakirudishiana maneno baina yao, kila mmoja anamtupia lawama mwingine, utaona jambo la kutisha! Watakuwa waliokuwa wakifanywa wanyonge wakisema kuwaambia wale waliokuwa na kiburi, nao ni wale viongozi na wakubwa waliopotea na kupoteza, «Lau si nyinyi kutupoteza njia tungalikuwa ni wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.» |