Quran with Swahili translation - Surah Saba’ ayat 37 - سَبإ - Page - Juz 22
﴿وَمَآ أَمۡوَٰلُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُم بِٱلَّتِي تُقَرِّبُكُمۡ عِندَنَا زُلۡفَىٰٓ إِلَّا مَنۡ ءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَأُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ جَزَآءُ ٱلضِّعۡفِ بِمَا عَمِلُواْ وَهُمۡ فِي ٱلۡغُرُفَٰتِ ءَامِنُونَ ﴾
[سَبإ: 37]
﴿وما أموالكم ولا أولادكم بالتي تقربكم عندنا زلفى إلا من آمن وعمل﴾ [سَبإ: 37]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hayakuwa mali yenu na watoto wenu ni vitu vya kuwafanya nyinyi muwe karibu na sisi, na daraja zenu ziwekwe juu, lakini wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na wakafanya matendo mema, basi hao watapata malipo ya nyongeza: kwa jema moja kwa kumi mfano wake mpaka kiwango cha nyongeza Anachokitaka Mwenyezi Mungu. Na wao watakuwa kwenye Pepo ya juu kwa juu, wakiwa wamesalimika na adhabu, kifo na mambo ya huzuni |