Quran with Swahili translation - Surah FaTir ayat 1 - فَاطِر - Page - Juz 22
﴿ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ فَاطِرِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ جَاعِلِ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ رُسُلًا أُوْلِيٓ أَجۡنِحَةٖ مَّثۡنَىٰ وَثُلَٰثَ وَرُبَٰعَۚ يَزِيدُ فِي ٱلۡخَلۡقِ مَا يَشَآءُۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ ﴾
[فَاطِر: 1]
﴿الحمد لله فاطر السموات والأرض جاعل الملائكة رسلا أولي أجنحة مثنى وثلاث﴾ [فَاطِر: 1]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sifa njema zote asifiwe Mwenyezi Mungu kwa sifa Zake ambazo zote ni za ukamilifu, na kwa neema Zake za nje na za ndani, za Akhera na duniani. Muumba mbingu na ardhi na Muanzilishi wa hizo. Mwenye kuwafanya Malaika ni wajumbe kwa waja kwa Anayemtaka miongoni mwa waja Wake, na kwa amri Yake anayoitaka na makatazo Yake. Na miongoni mwa ukubwa wa uweza wa Mwenyezi Mungu ni kuwafanya Malaika ni wenye mbawa, mbilimibili, tatutatu na nnenne, za kurukia: ili kukifikisha Alichoamrisha Mwenyezi Mungu. Katika uumbaji Wake Anaongeza Anachotaka. Hakika Mwenyezi Mungu kwa kila jambo ni Mjuzi, hakuna kitu kinachomshinda |