×

Hakika Sisi tunawafufua wafu, na tunayaandika wanayo yatanguliza, na wanayo yaacha nyuma. 36:12 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Ya-Sin ⮕ (36:12) ayat 12 in Swahili

36:12 Surah Ya-Sin ayat 12 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Ya-Sin ayat 12 - يسٓ - Page - Juz 22

﴿إِنَّا نَحۡنُ نُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَنَكۡتُبُ مَا قَدَّمُواْ وَءَاثَٰرَهُمۡۚ وَكُلَّ شَيۡءٍ أَحۡصَيۡنَٰهُ فِيٓ إِمَامٖ مُّبِينٖ ﴾
[يسٓ: 12]

Hakika Sisi tunawafufua wafu, na tunayaandika wanayo yatanguliza, na wanayo yaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari asli lenye kubainisha

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إنا نحن نحيي الموتى ونكتب ما قدموا وآثارهم وكل شيء أحصيناه في, باللغة السواحيلية

﴿إنا نحن نحيي الموتى ونكتب ما قدموا وآثارهم وكل شيء أحصيناه في﴾ [يسٓ: 12]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hakika sisi ndio tunaohuisha wafu wote kwa kuwafufua Siku ya Kiyama, na tunaandika waliyoyafanya ya kheri na shari, na zile athari zao njema ambazo wao walikuwa ndio sababu ya kufanyika katika maisha yao na baada ya kufa kwao, ziwe njema kama vile mtoto mwema, elimu yenye manufaa na sadaka yenye kuendelea, na ziwe mbaya kama vile ushirikina na uasi. Na tumedhibiti kwa hesabu kila kitu katika Kitabu chenye ufafanuzi, ambacho ni Asili ya Kitabu, na humo ndio marejeo ya yote hayo, nacho ni Ubao Uliohifadhiwa. Basi ni juu ya mwenye akili airudie nafsi yake, ili awe ni kiigizo katika wema ndani ya maisha yake na baada ya kufa kwake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek